Luke 17

1Yesu akawaambia wanafunzi wake, “mambo yasababishayo watu watende dhambi hayana budi kutokea, Lakini ole wake mtu anayeyasababisha! 2Ingekua ni heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe zito la kusagia shingoni na kutubwa baharini, kuliko kumfanya mmoja wa hawa wadogo atende dhambi.

3Jilindeni. Kama ndugu yako akikukosea mwonye, naye akitubu msamehe. 4Kama akikukosea mara saba kwa siku moja na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, ‘ninatubu,’ msamehe!”

5Mitume wake wakamwambia Bwana, “tuongezee imani yetu.” 6Bwana akasema, “kama mgekuwa na imani kama punje ya haradarii, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘n’goka na ukaote baharini,’ nao ungewatii.

7Lakini nani miongoni mwenu, ambaye ana mtumishi anayelima shamba au anayechunga kondoo, atamwambia arudipo shambani, ‘Njoo haraka na keti ule chakula? 8Je hatamwambia, ‘Niandalie chakula nile, na jifunge mkanda na unitumikie mpaka nitakapo maliza kula na kunywa. Baada ya hapo uta kula na kunywa?

9Hata mshukuru mtumishi huyo kwasababu katimiza yale aliyoamriwa? 10Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa semeni ‘Sisi tu watumishi tusiostahili. Tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.’

11Ilitokea kwamba alivyokua akisafiri kwenda Yerusalemu, alipita mpakani mwa Samaria na Galilaya. 12Alipokua akiingia kwenye kijiji kimoja, huko alikutana na watu kumi waliokuwa na ukoma. Wakasimama mbali 13wakapaza sauti wakasema “Yesu, Bwana tuhurumie.”

14Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” nao walipokua wakienda wakatakasika. 15Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa sauti kuu akimsifu Mungu. 16Akapiga magoti miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikua msamaria.

17Yesu akajibu, akasema, “Je hawakutakasika wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? 18Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumtukuza Mungu, isipokuwa huyu mgeni?” 19Akamwambia, “Inuka na uende zako imani yako imekuponya.”

20Alipoulizwa na mafarisayo ufalme wa Mungu utakuja lini, Yesu akawajibu akisema, “Ufalme wa Mungu sio kitu ambacho kinaweza kuonekana. 21Wala watu hawatasema, ‘Angalia hapa!’ au, ‘Angalia kule!’ kwa maana ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”

22Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona moja ya siku ya Mwana wa Adamu, lakini hamtaiona. 23Watawaambia, ‘Angalia, kule! Angalia, hapa!’ Lakini msiende kuangalia, wala kuwafuafata, 24kama umeme wa radi umulikao katika anga kuanzia upande mmoja hadi mwingine. Hivyo hata Mwana wa Adamu atakuwa ivyo katika siku yake.

25Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki. 26Kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokua katika siku ya Mwana wa Adam. 27Walikula, walikunywa, wakioa na kuolewa mpaka siku ile ambayo Nuhu alipoingia katika safina na gharika ikaja na kuwaangamiza wote.

28Ndivyo ilivyokua katika siku za Lutu, walikula, kunywa, wakinunua na kuuza, kulima na walijenga. 29Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma, ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka mbinguni ikawaangamiza wote.

30Hivyo ndivyo itakavyo kuwa siku ile ya Mwana wa Adamu atakapofunuliwa. 31Siku hiyo, usimruhusu aliye kwenye dari ya nyumba ashuke kuchukue bidhaa zake ndani ya nyumba. Na usimruhusu aliyeko shambani kurudi nyumbani.

32Mkumbuke mke wa Lutu. 33Ye yote anaejaribu kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini ye yote atakayeyapoteza maisha yake atayaokoa.

34Nakwambia, usiku huo kutakua na watu wawili katika kitanda kimoja. Mmoja atachukuliwa, na mwingine ataachwa. 35Kutakua na wanawake wawili wanasaga nafaka pamoja, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.” 36

Wakamwuliza, “Wapi, Mungu?” Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, ndipo tai hukusanyika kwa pamoja.”

37

Copyright information for SwaULB